Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, linawashikilia watu sita wanaohisiwa kuwa ni majambazi wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya mlinzi wa duka, Alex Patakiri (25), kisha kuiba baadhi ya vitu dukani hapo.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo amesema tukio hilo lilitokea Februari 28, 2023 katika eneo la Lulanzi, lililopo Kata ya Picha ya Ndege Wilayani Kibaha.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo.

Amesema, “walimvamia mlinzi huyo na kumuua na kisha kuiba vitu mbalimbali ambapo Polisi kwa kushirikiana na raia walikamata watuhumiwa hao pamoja na vitu vilivyoibwa na watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili baada ya upelelezi kukamilika.”

Katika tukio jingine, Kamanda Lutumo amesema Polisi imefanikiwa kuokoa mali za wananchi zilizoibwa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Pwani, ikiwemo pikipiki tatu, kukamata dawa za kulevya aina ya Heroin kete 14, bangi puli 48 na kete 382, magodoro na milango miwili ya nyumba.

Sakata la maandamano Kenya: Odinga akubali kiaina matakwa ya Ruto
Wagonjwa 80 wapatiwa rufaa uchunguzi, upasuaji wa moyo