Mkurugenzi wa Mashindano wa Young Africans, Saad Kawemba ametangaza kiama kwa kusema kuna michezo mitatu tu muhimu mbele yao ambayo wanataka ushindi ili waweze kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwenye msimamo wa Ligi Young Africans inaongoza kwa alama 65 baada ya kucheza michezo 24 ambapo imeshinda 21, sare mbili na kufungwa moja ikiwa na jumla ya mabao 34, huku Simba SC ikiwa nafasi ya pili na alama 57 ikiwa imeshinda michezo 17, sare sita na ikifungwa mmoja.

Kawemba amesema, kwenye tatu zijazo wanahidaji ushindi kwa hali na mali ili waweze kutangaza mabingwa mapema iwezekanavyo, ili wanaposhiriki kimataifa wasiwe na hofu ya ubingwa.

“Nataka ubingwa ndani ya mechi tatu zijazo pamoja na ya Simba, hivyo wanatakiwa kujua kuwa mechi zote tatu zijazo ni fainali kwetu hivyo hatutahitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi.”

“Tunajua dabi ni ngumu ila kwa kuwa kwetu tunahitaji kuhitimisha mjadala wa ubingwa mapema, hatuna sababu ya kutufanya tusizingatie nia yetu ya kuhakikisha tunatangazwa mabingwa ndani ya mechi tatu zijazo,” amesema Kawemba.

Simba SC na Young Africans zinatarajiwa kukutana April 16 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku timu hizo zikiwa na msimu miwili mfululizo hazijafungana katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo April 9, 2023
Huyu Ahmed Ally na Simba yake ni balaa