Watu wasiojulikana ambao walikuwa wamebeba silaha wamewateka watu 80, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto katika jimbo la Zamfara, lililopo eneo ambalo ni maarufu kwa matukio ya utekaji wa mara kwa mara nchini Nigeria.

Tukio hilo, limetokea Aprili 8, 2023 katika kijiji cha Wanzamai, na kuthibitishwa na wanakijiji ambao wamesema watendaji wa tukio hilo, walikuwa wamejihami kwa silaha.

Msemaji wa polisi katika jimbo la Zamfara, Mohammed Shehu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ingawa hajasena ni watu wangapi waliotekwa na watu hao wenye silaha.

Hata hivyo, wenyeji wa eneo hilo wanasema mpaka sasa watekaji hao hawajaomba fedha ili kuwaachia huru raia hao na kwamba kinachosubiriwa ni tamko lao ama Serikali kuchukua hatua na kuwakomboa.

Usiyoyajua kuhusu Siku kuu ya Pasaka Duniani
Kama Ripoti ya CAG ni nzuri, Rais nae ni mzuri