Taifa la Kenya, hii leo Aprili 10, 2023 inatarajiwa kuzindua setilaiti yake ya kwanza iliyopewa jina Taifa 1, itarushwa kwa kutumia roketi ya SpaceX falcon 9, kutokea kwenye kituo chake cha Vandenberg Space mjini Carlifonia nchini Marekani.

Taarifa kutoka kituo cha anga cha Kenya, imesema katika tukio la kihistoria kupitia mpango wake wa masuala ya anga inaleta umuhimu katika maendeleo ya teknolojia kwa taifa hilo na kwamba itachangia katika mpango wake wa kujenga uchumi kupitia anga.

Kenya inatarajia kuzindua setilaiti yake ya kwanza hii leo. Picha ya Chris O’Meara/AP.

Wizara ya ulinzi ya Kenya, imesema satellite hiyo imebuniwa na kutengenezwa na wahandisi wa Kenya na kwamba itatumika kukusanya takwimu kuhusu kilimo na usalama wa chakula miongoni mwa mambo mengine.

Hata hivyo, kurushwa kwa kifaa hiki, kutaongeza chachu ya maendeleo ya kisayansi na ubunifu kwa bara la Afrika, ambapo nchi ya Misri, ndio ilikuwa taifa la kwanza kufanya hivyo mwaka 1998.

Vijana wasio na wake, wasiooa kulipiwa Mahari
Papa Francis aombea amani, ataka watu kuaminiana