Taasisi ya Kiislamu ya Al- Hikma Foundation imetangaza kuwalipia mahari vijana 50 ambao wanahitaji kuoa.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sheikh Nurdin Kishki amesema mahari hiyo haitawahusu wale wanaotaka kuongeza mke wa pili.

Amesema, “tutafanya ndoa ya pamoja ya watu 50 mahari tutatoa Sisi Al-Hikma Foundation masharti usiwe unaongeza mke wa pili ndoa itafanyika Dar es salaam chini ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir.”

Hata hivyo, sharti hilo limewekwa kwa asiye na mke na sio lengo lake kusaidiwa wanaotaka kuongeza mke wa pili.

Rais Samia apongezwa uchukuaji hatua ripoti ya CAG
Kenya kuzindua Sattelite yake ya kwanza leo