Mwanamuziki Maarufu wa Dansi nchini Hussein Jumbe amefariki Dunia hii leo (Aprili 10, 2023), katika Hospitali ya Aman jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Majirani na Ndugu wa karibu wa Marehemu, wamesema Jumbe amefariki jioni ya leo katika Hospitali hiyo alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Enzi za uhai wake, Jumbo amewahi kutamba na tungo zake mahiri zikiwemo Nachechemea (akiwa na DDC Mlimani Park Orchestre), Siri ya nini (kama solo artist), Gunia la Mazoezi (akiwa na TOT Plus), Mlinzi wa Godown (akiwa na Mikumi Sound ya Morogoro), Kiapo (akiwa na OTTU Jazz Band) nk.

Mwanamuziki huyo nguli aliyejaaliwa vipaji adhimu vya sauti ya uimbaji, utunzi uliojaa hisia na zinazosisimua ambazo mara nyingi hugusa kila rika, alipata elimu yake ya msingi katika Shule za Uhuru Mchanganyiko na Sekondari ya Muslim, zote za jijini Dar es Salaam.

Taarifa zaidi kuhusu Mwanamuziki huyu na taratibu nzima za Maziko zitakuijia hivi punde, tafadhali usiache na endelea kufuatilia page za Dar24 Media.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo April 11, 2023
Kuvunja bodi ya TRC pekee haitoshi: CHADEMA