Bunge la Iran linatarajia kuidhinisha mapendekezo ya kutoa adhabu kali kwa wahusika wa ukatili dhidi ya wanawake, mapendekezo ambayo yanaweza kupitishwa na kuwa sheria ndani ya miezi michache.

Majadaliano hayo ya Bungeni yaliyoanzishwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, yamepelekea kupitishwa kwa kanuni za jumla za mswada uliotajwa kuwa wa kuzuia madhara kwa wanawake na kuboresha usalama wao dhidi ya tabia mbaya.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Serikali – IRNA, muswada huo ambao unaweza kufanyiwa marekebisho, unaweza kusainiwa rasmi na kuwa sheria katika miezi ijayo.

Hata hivyo, Mchakato huo unajiri ikiwa ni takriban miezi saba baada ya maandamano ya nchi nzima yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini kilichotokea mwezi Septemba akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.

Viwanja saba kufanyiwa ukarabati Tanzania Bara
Hussein Jumbe kupumzishwa Makaburi ya Kisutu