Mazishi ya mwimbaji na mtunzi mahiri wa muziki wa Dansi, Hussein Jumbe yanatarajia kufanyika hi leo (Jumanne/ April 11, 2023), katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Jumbe ambaye alifariki hapo jana jioni (Jumatatu/ Machi 10, 2023) katika hospital ya Amana, Ilala akisumbuliwa na maradhi ya Vidonda vya Tumbo na kifua kwa muda mrefu.

Msiba wa marehemu Hussein Jumbe, upo nyumbani kwake eneo la Kigamboni Toangoma ambapo mwili wake utafikishwa katika msikiti Maamur uliopo Upanga wakati wa sala ya Alasiri kabla kuelekea makaburi ya Kisutu kumpumzisha.

Jumbe aliyekuwa akiitwa Mzee wa Dodo, aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde Ngona ya Ukae’, TOT Plus, OTTU Jazz na Mikumi Sound, ambapo hadi anafariki alikuwa akimiliki kundi lake la Talent Band.

Bunge laidhinisha sheria adhabu kali ukatili dhidi ya Wanawake
Serikali yasitisha ajira Wafanyakazi wa Afya