Beki wa Kati kutoka Visiwani Zanzibar Ibrahim Hamad ‘Bacca’ amegeuka Lulu na kutumiwa kama mfano katika kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans ambacho kinaendelea kupepea kwa ushindi katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Bacca amekuwa katika kiwango Bora tangu alipoanza kuaminiwa kwenye kikosi cha Mabingwa hao, hali ambayo imemlazimu Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kuwawataka wachezaji wa timu hiyo, kufuata mfumo wa beki huo.

Kocha Nabi amesema anataka kuona wachezaji wote wakipambana na kuonesha ushindani wa namba kama ilivyokuwa kwa Bacca.

Nabi amesema Bacca ni somo tosha kwa wachezaji wengine ambao wanapewa nafasi na kushindwa kuonesha kiwango bora.

Aliongeza kuwa, anataka kuona ushindani ukiongezeka kwa kila mchezaji pale

“Ushindani wa namba unapokuwepo kunanipa wigi mpana wa kuchagua mchezaji gani wa kumtumia katika kikosi changu cha kwanza.”

“Ninafurahia kiwango kizuri ambacho Bacca amekionesha tangu nianze kumuamini na kumpa nafasi ya kucheza.”

“Tangu ameingia katika kikosi cha kwanza hajatoka hadi hivi sasa, nakumbuka aliingia katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir kwenye Uwanja wa Mkapa,” amesema Nabi.

Kauli hiyo huenda ikawa kama kijembe kwa baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakipewa nafasi ya kucheza, lakini hawadumu katika kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa kwa Bacca.

Wachezaji baadhi ambao wamekuwa wakipewa nafasi ya kucheza na kushindwa kudumu ni Dickson Ambundo, Chrispin Ngushi na David Bryson.

Wydad Casablanca kushuhudia Kariakoo Dabi
Rivers United kubadili Uwanja Nigeria