Mkurugenzi wa Michezo wa Mabingwa wa Soka nchini Italia AC Milan, Frederic Massara amesema wana mpango wa kufanya mazungumzo na Real Madrid kwa ajili ya kumsajili Brahim Diaz.

Diaz amekuwa ndani ya Milan kwa muda mrefu akicheza kwa mkopo akitokea Real Madrid ambapo mwisho wa msimu huu atatakiwa kurudi Santiago Bernabeu.

Diaz huu ukiwa ni msimu wake wa tatu kikosini hapo, amekuwa akipambana ambapo msimu uliopita aliipa Milan ubingwa wa Serie A.

Milan sasa inataka kumsajili moja kwa moja nyota huyo ifikapo mwishoni wa msimu huu mkataba wake wa mkopo utakapomalizika.

Massara alisema lengo lao ni kuona Diaz anaendelea kusalia kikosini hapo ndiyo maana wanataka kufanya mazungumzo na Madrid.

Kocha Rivers United aichimba mkwara Young Africans

“Najua mkopo wa Brahim unamalizika, amekuwa akifanya vizuri tangu amekuwa hapa, tunataka kuongea na Real Madrid.

“Tunataka kuona anaendelea kuwa hapa, ngoja tusubiri kuona Real Madrid wao wana masharti gani au watasema nini kuhusu Brahim.”

Mjadala wa uchumi: Wabunge Chama tawala kukutana na wapinzani
Eduardo Camavinga aishika pabaya Real Madrid