Beki na Nahodha wa Manchester United, Harry Maguire amefunguka kwa kitendo cha kukosa muda wa kucheza Old Trafford, lakini amesisitiza kuwa atapambana na wenzake ili kuhakikisha wanashinda zaidi ya mataji mawili msimu huu.
Maguire ameona vigumu kuvumilia kukaa kwenye Benchi kwa muda mrefu ukizingatia yeye ni nahodha namba moja ingawa msisitizo wake ni kuwa anataka kuwasaidia wenzake kuwa mabingwa.
Maguire ambaye ameanza kwenye michezo sita tu ya Ligi Kuu ya England msimu huu 2022/23, mwishoni mwa juma lililopita aliiongoza United kushinda mabao 2-0 dhidi ya Everton.
“Nataka kucheza kila mchezo na nimefanya hivyo kwa miaka nane iliyopita ya maisha yangu ya soka.”
“Pia, lazima nimuheshimu kocha na maamuzi yake na pia kuheshimu jinsi ushindani ulivyo mzuri katika safu ya beki wa kati katika klabu hii. Ndivyo, na ninaamini hivyo.”
“Sikiliza, ninapopata nafasi, nataka kucheza, nataka kushinda na muhimu zaidi kwa timu, kuwa na ushawishi kwenye mchezo.”
“Bila shaka nataka kucheza kila mchezo na nina uhakika kama ungezungumza na mabeki wetu wa kati katika majukumu yao, wote wana uzoefu na wamecheza katika kiwango cha juu na wote watakata tamaa wanapokuwa kwenye benchi.” amesema Beki huyo