Mapigano mapya kati ya makundi mawili ya waarabu na waiso waarabu, katika eneo la Darfur nchini Sudan yamesababisha vifo vya watu 24, nyumba kadhaa kuchomwa moto na maelfu ya watu kukimbia makazi yao.

Ghasia hizo za karibu na mpaka na Chad, zimeripotiwa kuzuka kati ya makundi ya kabila la waarabu na Masalit katika mji wa Foro Baranga, umbali wa kilomoita 185 kutoka mji mkuu wa Jimbo la Darfur Magharibi, Geneina.

Kiongozi wa Baraza la Foro Baranga, Mohammed Hussein Teema amesema mapigano hayo yalizuka jumamosi iliopita ambapo karibu nyumba 50 za eneo hilo zilichomwa moto na kusababisha familia 4,000 kukosa makaazi.

Machafuko hayo, yameifanya mamlaka wa Sudan kutangaza marufuku nyakati za usiku pamoja na hali ya dharura kwa kipindi cha mwezi mmoja katika jimbo hilo, na hali ya usalama inaelezewa kuanza kuimarika baada ya maafisa wa usalama kupelekwa Foro Baranga.

Sawadogo arudisha jibu kwa wanaombeza
Mwenyekiti SPUTANZA afunguka kesi ya Fei Toto