Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya AC Milan, Olivier Giroud atasaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo wakati wowote kuanzia sasa, huku akitarajia kulipwa mshahara wa Euro Milioni 3.5 kwa mwaka.

Giroud yupo ndani ya AC Milan huu ukiwa ni msimu wake wa pili tangu alipouzwa na Chelsea mara baada ya kutwaa taji la Ulaya.

Mkataba wa Giroud wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu kikosini hapo.

Milan inatarajiwa kumpatia mkataba wa mwaka mmoja ambao ni mpaka Juni 2024, huku mshahara wake wa mwaka utakuwa ni euro 3.5m. Katika usajili wa Januari mwaka huu, Everton kutoka Premier League ilijaribu kutaka kumsajili straika huyo.

Giroud tangu ametua Milan amefanikiwa kuipa timu hiyo ubingwa wa Serie A. Straika huyo ni kati ya wachezaji ambao wamefanikiwa kushinda mataji makubwa kama Kombe la Dunia na Ligi ya Mabingwa.

Marco Reus kulamba dili la Euro Milion 7
Baadhi ya watoa huduma za afya ni wadanganyifu: Dkt. Mollel