Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema hapendezwi na kitendo cha barabara kufungwa kwa masaa mengi ili apite, na kwamba tayari ameshamuambia Mkuu wa Jeshi Polisi nchini IGP kuwa kitendo hicho kinazuia shughuli za Wananchi.

Dkt. Mpangop ameyasema hayo wakati akiwa Wilayani Magu na kuwaomba radhi Wananchi juu ya kitendo hicho akisema haifai kufunga barabara kwa masaa manne ili yeye apite na kwamba dakika 10 zinatosha ili Wananchi waendelee na shughuli zao.

Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango.

Amesema, “Nilishamwambia IGP na nirudie kuwaambia Makamanda wa Polisi wa Mikoa, mambo ya kufunga Barabara kwa masaa mengi kisa tu Mtoto wa masikini Philip Mpango anapita hapana, sitaki kusikia tena hili linajirudia, masaa manne kweli?”

“Muambizane na wanaopokea msafara huko tutakakopita acheni Wananchi wapite kwani dakika 10 hazitoshi), masaa manne kweli!?, nawaomba radhi ya dhati kabisa Wananchi,” amesema Makamu wa Rais, Dkt. Mpango.

FC Barcelona yaisafishia njia Man Utd
Halmashauri zatakiwa kutenga bajeti ununuzi wa Miche