Kiungo Mshambuliaji kutoka Ujerumani Leroy Sane ameuomba uongozi wa Bayern Munich kutompa adhabu Sadio Mane kufuatia kitendo chake cha kumpiga ngumi mdomoni, baada ya mchezo wa Robo Fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City.

Hata hivyo Mane amesimamishwa na uongozi wa klabu hiyo kutokana na tukio hilo lililotokea nje ya uwanja wa Etihad mjini Manchester baada ya kuchezea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Manchester City.

Bayern ilithibitisha kwamba Mane hatakuwa sehemu ya mchezo muhimu wa Bundesliga dhidi ya Hoffenheim unaochezwa leo Jumamosi (April 15) katika uwanja wa Allianz Arena.

Inadaiwa kuwa Leroy Sane ambaye aliwahi kuitumikia Man City anataka kuweka tukio hilo kando na kusahau yaliyotokea kumuombea radhi.

Sane anataka akili zao zifikirie zaidi malengo ya msimu huu ikiwamo kubeba ubingwa wa Bundesliga baada ya kuboronga kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na gazeti kutoka Ujerumani SPORTI, Sane alizungumza na uongozi wa klabu kuhusu ishu yake na Mane, akisisitiza wasimpe adhabu nzito Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal, inaaminika mtendaji mkuu, Oliver Khan na mkurugenzi wa michezo, Hasan Salihamidzic, wanataka kuona mwenendo mzuri wa Mane ambaye huenda akaondoka endapo kiwango chake hakitawaridhisha.

Mane amefunga mabao 11 na kutengeneza asisti tano tangu alipojiunga na Bayern akitokea Liverpool katika dirisha la usajili la kiangazi lililopita.

Mohammed Ouattara aondoka kambini SImba SC
Baleke amuibua mshambuliaji Young Africans