Chama cha Soka England ‘FA’ hakitampa adhabu mwamuzi wa akiba Constantine Hatzidakis kutokana na kumpiga kiwiko beki wa Liverpoool, Andy Robertson.

Hatzidakis alizua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana akimpiga kiwiko beki huyo kwenye mechi ya sare ya ma- bao 2-2 dhidi ya Arsenal.

Robertson na mwamuzi huyo walionekana wakijibizana maneno wakati wachezaji walipokuwa wakielekea mapumziko kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu England uliochezwa katika Uwanja wa Anfield.

Baada ya tukio hilo waamuzi waliochezesha mchezo huo walizungukwa na wachezaji wa Liverpool sambamba na Robertson ambaye alikuwa na hasira na kuishia kuzomewa na mashabiki.

Hata hivyo, FA imethibitisha kuwa hakuna adhabu itakayotolewa dhidi ya mwamuzi huyo baada ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

“Tumerudia tukio zima huku tukiwa na ushahidi wa kutosha. Mchakato wetu wa kina ulihusisha kukagua taarifa za kina kutoka Liverpool na Chama cha Waamuzi England (PGMOL) pamoja na mikanda ya video kuhusiana na tukio hilo na mazingira yake.

“FA imeamua kutompa adhabu baada ya kujiridhisha,” hiyo ilikuwa kauli ya FA kupitia vyombo vya habari Wiki iliyopita wachambuzi wa soka walishinikiza mwamuzi huyo afungiwe kufuatia tukio hilo lililotokea kwenye mchezo huo.

Mchambuzi wa soka, Darrent Bent alisisitiza mwamuzi huyo afungiwe zaidi ya mechi nane kutokana  do chake cha kumpiga kiwiko beki huyo wa Liverpool. “Haiwezekani.

Mwamuzi afungiwe mechi nane kama mchezaji wa Fulham, Aleksandar Mitrovic alivyofungiwa,” aliandika Bent kupitia akaunti yake ya Twitter.

Mchambuzi mwingine Chris Sutton, alidai: “Matukio kama haya hayakubaliki kwenye soka. Kwa hiyo adhabu itolewe haraka iwezekenavyo.”

Chama, Saido wakabidhiwa kazi nzito Simba SC
Zijue harakati za kutafuta sheria bora ya Habari