Mabondia 24 wa ngumi za kulipwa nchini, watapanda ulingoni Jumamosi (April 22) kabla ya Bondia Twaha Kiduku kuzichapa na Lago Kiziria kutoka nchini Georgia.

Pambano linalojulikana kama ‘Mfalme Katika Ufalme Wake’, linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Tanzanite, mkoani Morogoro.

Promota wa pambano hilo, Meja Selemani Semunyu amesema mapambano ya utangulizi yatakuwa 12 yenye ushindani mkubwa, kutokana na rekodi za mabondia watakaopanda ulingoni.

“Mapambano 12 ya utangulizi yatakuwa moto kwa sababu mabondia wanaocheza mahiri wanapokuwa wana vipaji na ulingoni,” amesema Semunyu

Semunyu ametaja baadhi ya mapambano hayo ni kati ya Said Mkola na Habibu Pengo, Ally Ngwando kuzichapa na Jamal Kunoga, Juma Choki ataonyeshana ubabe na Loren Japhet wakati Joseph Mchapeni atapimana uwezo na Emmanuel Mgogo.

Bondia Juma Choki, amesema anaendelea kujipanga vizuri kuhakikisha anaonyesha uwezo wa hali ya juu katika pambano hilo.

Frank Lampard achimba mkwara Chelsea
Ally Salim aweka rekodi mpya Kariakoo Dabi