Mshambuliaji Kylian Mbappe amekuwa mfungaji bora wa muda wote wa Klabu Bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo ‘Ligue 1’, huku mabingwa hao wa Ufaransa wakipiga hatua kubwa kuelekea kulitwaa taji.

PSG iliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Lens wanaoshika nafasi ya pili kwenye Uwanja wa Parc des Princes jijini Paris juzi Jumamosi (April 15).

Mbappe, ambaye tayari ni mfungaji bora wa PSG katika michuano yote, alifunga bao lake la 139 katika Ligue 1 dakika ya 31 na kumpiku Edinson Cavani.

Kufikia hatua hiyo, Lens tayari ilikuwa imepunguzwa hadi wachezaji 10 baada ya kadi nyekundu ya dakika ya 19 kwa Salis Abdul Samed kwa kumchezea vibaya Achraf Hakimi.

Wenyeji walijihakikishia ushindi kabla ya muda wa mapumziko kutokana na mabao zaidi ya Vitinha na Lionel Messi.

Vichapo vya mfululizo vya hivi majuzi kwa PSG vimeifanya Lens iliyo katika kiwango chake kufunga pengo kileleni mwa Ligue 1 hadi pointi sita pekee.

Lakini vijana wa Christophe Galtier walifanya kazi nyepesi kwa wapinzani wao Jumamosi kuongeza faida yao hadi alama tisa huku kukiwa na mechi saba za msimu kumalizika.

Mafunzo Taasisi ya Empower kwa walimu yasitishwa
Kocha Kagera Sugar atahadharisha Ligi Kuu