Mshambuliaji wa Klabu ya SS Lazio ya Italia, Ciro Immobile jana Jumapili (April 16) alinusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari ambayo ilimlazimu kukimbizwa hospitali kwa ajili ya vipimo ambapo iligundulika hakuumia kwa ndani licha ya kuwa na maumivu madogo ya mguu.

Nyota wa Italia mwenye umri wa miaka33, alipata ajali hiyo akiwa akiwa anendesha gari lake la Land Rover SUV ambapo alikuwa na watoto wake wawili wakike, ajali ambayo ilitokea mita chache karibu na uwanja wa Lazio, Stadio Olimpico.

Muda mfupi baada ya ajali hiyo, Immobile aliimbia AGTW kuwa: “Nashukuru niko sawa, japo mguu una maumivu kidogo.”

Immobile alipata ajali hiyo ikiwa ni siku mbili tu baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Spezia Ijumaa iliyopita.

Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji na usafishaji madini
Mchungaji wa mfungo uliouwa wanne aondolewa dhamana