Raia wa Marekani, Hans Nilson Langseth ndiye binadamu pekee aliyewahi kuwa na ndevu ndefu zaidi duniani zikiwa na urefu wa futi 17 na inchi 5.
katika maisha yake, alianza kufuga ndevu kama sehemu ya mashindano na alishinda huku katika maisha yake akitumia muda mwingi kusafiri kote nchini Marekani kwa maonesho ya ndevu zake.
Hans Langseth.
Binadamu huyu aliyeweka Historia na kuzusha mijadala mbalimbali katika jamii, alizaliwa July 14, 1846 na alifariki – November 10, 1927 baada ya kuzikanyaga ndevu zake na kuvunjika shingo.
Alifariki akiwa na umri wa miaka 81, huko Wyndmere, Dakota Kaskazini, na akazikwa katika Makaburi ya Kanisa la Elk Creek ya mji wa Kensett, Iowa na hadi anafariki ndevu zake zilikuwa na urefu wa mita 5.33 (futi 17.5).
Msichana mdogo akiwa katika jaribio la kuruka ndevu za Hans Langseth. Picha ya Flickr.