Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waendelee kufanya kazi Weledi, Ubunifu na bidii ili kuchochea maendeleo ya haraka yenye matokeo chanya kwa Watanzania.

Waziri Mkuu, ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo na taasisi zilizo chini yake kwenye hafla fupi ya futari aliyoiandaa kwa ajili yao, Mlimwa, jijini Dodoma. 

Amesema, “nitumie fursa hii kuwapongeza kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa shughuli za serikali. Natoa pongezi kwa uwajibikaji mzuri na pia naungana nanyi kumuahidi Mheshimiwa Rais wetu kuwa tutafanya kazi bidii zaidi.”

Aidha, Waziri Mkuu pia amewataka watumishi hao waendelee kuhakikisha Serikali inapata mafanikio. “Tuna jukumu la kumwezesha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa kusimamia miradi yote ya maendeleo. Sisi ndiyo tunapaswa kuratibu na kusimamia miradi ili ifanikiwe” amesema.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi wa Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amewataka watumishi hao waendelee kutunza heshima ya Ofisi pamoja na kumuwezesha Mheshimiwa Waziri Mkuu kumsaidia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan majukumu ipasavyo.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amesema watumishi wanapaswa kuendelea kufanya kazi upendo ukarimu na mshikamano ili nchi uweze kufanikiwa.

JKT Tanzania: Ubingwa Championship ni suala la muda
Arsene Wenger aipa mbinu za ubingwa Arsenal