Aliyewahi kuwa Meneja wa kikosi cha Arsenal Arsene Wenger amesema Arsenal wanatakiwa kuifunga Manchester City ili kutwaa taji la Premier League msimu huu licha ya kuyumba hivi karibuni.

Arsenal kwa sasa wanapambana kuona wanafanikiwa kutwaa taji la Premier League kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.

Hivi karibuni, Arsenal imeshindwa kutamba katika michezo miwili mfululizo baada ya kutoa sare dhidi ya Liverpool kisha West Ham Utd, lakini bado ipo kileleni mwa msimamo.

Arsenal na Man City wamepishana alama nne, huku Man City wakiwa na mchezo mmoja mkononi. Aprili 26, mwaka huu timu hízo zitapambana kwenye Uwanja wa Etihad.

Wenger amefunguka kuwa, Arsenal wanatakiwa kupata ushindi kwa sasa katika michezo yake saba iliyosalia akieleza kuwa ubingwa upo mikononi mwao.

“Arsenal awali hawakuwa katika nafasi nzuri ya kushinda taji la ligi, lakini kwa sasa kuna matumaini makubwa msimu huu ni kushinda taji na msimu ujao na kama itashindika basi italeta tensheni kubwa.

“Arsenal wapo katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa, wanatakiwa kumfunga Man City na kushinda mechi zote zilizopo mbele yao, mchezo wa hawa wawili ndiyo unaweza kutoa picha halisi ya ubingwa kwa msimu huu.

“Arsenal nafasi wanayo kubwa na hawatakiwi kufanya makosa kwa sababu Man City wanaweza kufanya lolote,” amesema Wanger ambaye ndiye aliipa Arsenal ubingwa wa Premier mara ya mwisho bila ya kupoteza mechi hata moja msimu wa 2003/04.

Majaliwa ataka weledi, Ubunifu matokeo chanya kimaendeleo
Singida B.S: Hatuna papara na Young Africans