Kurasa za Mtandao wa Kijamii wa Twitter za Klabu kubwa nchini Tanzania Simba SC na Young Africans zimefutiwa Blue Tick ikiashiria kuanza kwa mchakato wa kulipia ili kupata huduma hiyo.

Twitter imenza mchakato wa kufuta Blue Tick tangu jana Alhamis (April 20) kama alivyotangaza mmiliki wa mtandao huo Elon Musk mnamo Aprili 11-2023.

Elon Musk alifikia maamuzi hayo kwa madai kwamba kuna watu walipata utambulisho huo kwa njia zisizo halali ikiwemo kutoa rushwa.

Awali Musk alitangaza kuwa utaratibu huo ungeanza Aprili Mosi, 2023 lakini baadae akatangaza kuwa Aprili 20 kuwa ndio siku ya kuanza kwa mchakato huo.

Young Africans yampandisha thamani Ally Salim
Ushirikiano kuinua sekta ya Uvuvi EAC - Silinde