Imefahamika kuwa Mlinda Lango chaguo la tatu Simba SC Ally Salim amesaini Mkataba mpya wa miaka mitatu baada ya kuonyesha kiwango kizuri dhidi ya Young Africans.

Ally Salim aliweka Rekodi ya kuitumikia Simba SC katika mchezo wa Jumapili (April 16) dhidi ya Young Africans, ambao ulimalizika kwa Mnyama kuibuka na ushindi wa 2-0.

Taarifa kutoka ndani ya Simba SC zinaeleza kuwa Salim amesaini mkataba hadi mwaka 2027 na atakuwa akilipwa Mshahara Shilingi Milioni 4, ambao ni nyongeza ya asilimia 50 ya Mshahara wa awali.

Mwanzoni mwa msimu huu 2022/23 Simba SC ilitaka kumtoa kwa mkopo, lakini Benchi la Ufundi likaona kuna umuhimu wa kuendelea kuwa naye, kutokana na maendeleo yake kuridhisha kikosini.

Hadi sasa Salim ameshaitumikia Simba SC katika Michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, akitangulia kukaa langoni kwenye mchezo dhidi ya Ihefu FC ambao ulimalizika kwa ushindi wa 2-0, katika Uwanja wa Highland Estate mkoani Mbeya.

Mo Dewji kutinga kambini Simba SC
Simba SC, Young Africans zafutiwa Blue Tick