FC Barcelona inaweza kuchukua hatua ya kumsajili, Lionel Messi, lakini La Liga haitabadilisha kanuni zake ili kusaidia hilo, kwa mujibu wa Rais wa Ligi Kuu Hispania, Javier Tebas.

Tebas ameonyesha nia ya kumwona mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina akirejea Hispania.

Messi, ambaye anachukuliwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa wakati wote, aliondoka Barca kwa uhamisho wa bure miaka miwili iliyopita baada ya vikwazo vya kifedha kuzuia klabu hiyo kumpa mkataba mpya.

Tangu wakati huo kumekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara kuhusu Messi kurejea kutoka Paris huku Saint-Germain, mkataba wake wa awali nchini Ufaransa ukikamilika mwishoni mwa msimu huu.

Lakini hali ya kifedha ya Barca bado haijaimarika kiasi kumrudisha namba 10 huyo.

Tebas aliwaambia Blaugrana mwezi uliopita watalazimika kurejesha kiasi kikubwa cha ada ya uhamisho na kupun mishahara guzwa kabla ya kufanya usajili wowote.

Kisa CAF, Uwanja wa Mkapa kufungwa Mei 2023
Aishi Manula achafua hali ya hewa Simba SC