Gwiji wa Soka nchini Tanzania Abdallah Kibadeni ‘King’ ameitaka timu yake ya Simba SC pamoja na watani zao Young Africans kupambana kusaka ushindi katika mechi zao za hatua ya Robo Fainali ya michuano ya kimataifa na kuvunja rekodi kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo.

Simba SC kesho Jumamosi (April 22) itashuka katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad wakati Young Africans itakuwa ugenini Nigeria ikiwakabili Rivers United.

King amesema kumbukumbu zake zinamwonyesha ni mara moja tu timu ya Simba SC ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Afrika lakini ilikuwa katika Kombe la Shirikisho hivyo msimu huu wajitume zaidi kuifikia au kuivunja rekodi hiyo.

“Nawapongeza Simba na Young Africans katika hatua nzuri waliyoifikia ya kucheza Robo Fainali, hivyo wanahitaji kujipanga upya katika mechi zao zinazofuata kwa ajili ya kuhakikisha tunapita katika hatua hii na kuvunja rekodi.”

Simba SC tulifika fainali ya Kombe la CAF, wakati huo nilikuwa nafundisha Simba, tulivyocheza kwao tulishinda, tuli- kuja kutolewa hapa nyumbani mbele ya Rais Mwinyi (Ali Hassan), wakati huo na Stella Abdijan ya Ivory coast, hivyo tukajikuta tumepoteza kombe,” amesema King

Mkongwe huyo aliongeza anatamani kuona Simba na Young Africans zinafanya vizuri zaidi msimu huu na kutimiza malengo yao ikiwa ni kuunga juhudi za Rais. Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Ukiangalia Rais Samia anavyotoa ahadi kwa kila goli na kuwapa motisha wachezaji, pia kuna wadau wanaofuatilia na kutoa ahadi, hivyo ni wajibu wao kupambana na kuvuka hatua ya robo fainali,” amesema King

Inzaghi: Ni kama ndoto kucheza nusu fainali
Kisa CAF, Uwanja wa Mkapa kufungwa Mei 2023