Meneja wa Inter Milan Simone Inzaghi, amekiri hapo awali alikuwa kama ndoto tu kwa timu yake kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Nerazzurri hao walijumuishwa katika kile kilichochukuliwa kundi la kifo mapema katika mchuano huo walipowekwa pamoja na Bayern Munich na Barcelona, na hivyo kufanikiwa kuwa washindi wa pili mbele ya wababe hao wa La Liga.

Inter Milan iliishinda Benfica kwa jumla ya mabao 5-3 baada ya sare ya 3-3 kwenye dimba la San Siro katika mechi ya hatua ya robo fainali ya pili iliyochezwa juzi.

Hivyo inamaanisha Inter itamenyana na wapinzani wao wa jiji moja, AC Milan katika nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2002/03.

“Kuna furaha kubwa,” Inzaghi alisema baada ya mchezo. “Tulicheza mchezo mzuri dhidi ya timu ngumu.

“Tulistahili kabisa nusu fainali hii, ambayo hapo awali ilikuwa ndoto tu. Nina furaha kwa vijana na kwa maendeleo yetu. Tulianza na kundi gumu sana na Barcelona na Bayern Munich. Tulifanya kazi kila siku ili kupata uzoefu.

PICHA: Young Africans yawasili salama Uyo
Kibadeni azipa mbinu Simba SC, Young Africans