Uongozi wa Klabu ya Chelsea umeripotiwa kuwasiliana na Meneja Mauricio Pochettino ili kwenda kuziba nafasi ya wazi ya katika Benchi lao la Ufundi huko Stamford Bridge.

Pochettino mwenye umri wa miaka 51, amekuwa hana kazi tangu alipofutwa kazi Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu uliopita na kilichoelezwa ni kwamba tangu Januari 2023 alikuwa kwenye rada za Chelsea.

Lakini, kwa sasa ameanza kuhusishwa na mpango wa kuchukua mikoba ya Graham Potter huko Stamford Bridge. Mabosi wa The Blues wamewasiliana na Pochettino juu ya kibarua hicho.

Meneja huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur ataungana na Julian Nagelsmann kwenye orodha ya mameneja wanaowindwa na Chelsea sambamba na Luis Enrique, ambaye juma lililopita alikutana na mabosi wa The Blues kujadili mpango huo licha ya sasa kuwa kimya.

Kama Chelsea wataamua kumchunia Enrique basi jambo hilo litatoa nafasi kwa Spurs, ambao pia wanampigia hesabu kocha huyo wa zamani wa  FC Barcelona licha ya mwenyekiti Daniel Levy kuwa na wasiwasi juu ya kukosekana kwa uzoefu wa Ligi Kuu England kwa Meneja huyo.

Meneja wa Sporting Lisbon, Ruben Amorim naye pia amekuwa akizungumzwa juu ya kwenda kuchukua mikoba ya kuinoa Chelsea.

Kuhusu Nagelsmann alijadili juu ya kuchukua kazi hiyo ya Stamford Bridge juma lililopita na imeelezwa amevutiwa na kazi ya kwenda kuinoa Chelsea.

Pochettino alifanyiwa usaili na wamiliki wa Chelsea, Todd Boehly na Behdad Eghbali kabla ya kumpa kazi Potter, ambaye amedumu na timu hiyo kwa miezi saba tu kabla ya kufutwa kazi.

Chelsea kwa sasa ipo chini ya kocha wa muda, Frank Lampard.

Meridianbet Kasino Yaja na  mchongo mpya
Naibu waziri mkuu Dominic Raab ajiuzulu