Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam Manispaa ya Bukoba wametoa Zakatir al Fitri ya vyakula kwa baadhi ya familia, ikiwa ni mojawapo ya nguzo ya Uislam ambayo hutolewa kabla ya swala ya Eid Al Fitri.

Akizungumza wakati wa utoaji wa Zaka hiyo, Mudir wa JASUTA kanda ya ziwa, Abdulshahid Abbas amewasisitiza waumini wa kiislam kutoa zaka kwani ni sehemu ya nguzo ya uislam na ina faida kwao mbele ya Mwenyezi Mungu.

Abdulshahid Abbas – Mudir wa JASUTA Kanda ya Ziwa.

Amesema, “wale ambao hawajatoa Zakatil Fitri tunawahasa na kuwaomba wafanye haraka kutoa kwasababu kuacha kutoa Zakatil Fitri ni sawa sawa na kucheza na Swaum yako, muda wa kutoa ni siku mbili kabla ya Eid na mda wa mwisho kutolea ni Siku ya Eid kabla ya swala ya Eid Al Fitri.”

Abbas ameongeza kuwa, “zaka hii ni zaka iliyotolewa na waislam, wametoa zaka yao wameamini kwamba kupitia hapa ni salama na leo sisi tunaigawa kuirudisha kwa waislam wenye haki katika zakatil Fitri.”

Waumini wa dini ya Kiislam msikiti mpya wa Buyekera wakipokea Zakatil Al Fitri.

Kwa upande wa familia zilizopokea sadaka hiyo ya Zakatil Fitri, wamewashukuru waumini hao na kuwatakia kheri na malipo mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Harry Maguire na wenzake kupigwa bei Man Utd
PICHA: Young Africans yawasili salama Uyo