Kichapo cha mabao 3-1 kutoka Mainz, kimemfanya Meneja wa Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Thomas Tuchel kuweka wazi kwa nini kikosi chake kimekuwa kikipoteza michezo yake.

Tuchel na kikosi chake hicho juzi Jumamosi (April 22) waliduwazwa na Mainz baada ya kuwapa kichapo cha mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ wakiwa ugenini katika Dimba la MEWA Arena.

Kichapo hicho kinakuwa cha tatu kwa Tuchel tangu akabidhiwe mikoba ya kuifundisha timu hiyo na cha pili katika Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’.

Baada ya kichapo hicho kwa sasa Bayern wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga wakipitwa na wapinzani wao Dortmund kwa alama moja, Dortmund wakiwa nazo 60 wakati Bayern wanazo 59.

Tuchel amesema: “Ni jambo lisilotegemewa sisi kupoteza mchezo ule. Hatukuwa makini sana.”

“Hatukuwa na nguvu ya kupambana pale ambapo Mainz walikuwa wanakuja langoni kwetu. Sijui kwa nini inakuwa hali hii.”

Mzamiru: Hatuyapi nafasi yanayosemwa, tutapambana
Xabi Alonso atishia nafasi ya Moyes West Ham Utd