Uongozi wa Young Africans umesema kuwa haijalishi ni matokeo gani ambayo wameyapata wakiwa nchini Nigeria kwani watahakikisha kila kitu kinakuwa vyema kwa kuutumia uwanja wa nyumbani vizuri ili kufanikisha malengo yao na kutinga katika hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans jana Jumapili (April 23) walicheza mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho BArani Afrika dhidi ya Rivers United ya nchini Nigeria huku mchezo wa marudiano Young Africans wakitarajiwa kuwa nyumbani katika Uwanja wa Mkapa, Dar Jumapili (April 30).

Akiwa safariki kurejea jijini Dar es salaam Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe amesema: “Haijalishi ni matokeo gani ambayo tutayapata tukiwa ugenini dhidi ya Rivers kwani mpira wa Afrika mara zote ni suala la nyumbani.”

“Hivyo lazima na sisi tuhakikishe kuwa katika uwanja wetu wa nyumbani tunapata matokeo mazuri ambayo yatatufanya tuweze kusonga mbele katika hatua ya Nusu Fainali.”

“Wapinzani wetu ni timu nzuri ambayo ukiwatazama utaona ni kwa kisai gani nao wanataka kuweka historia yao ya kuuzu Nusu Fainali, hivyo lazima kila mmoja achange karata zake vyema na sisi tunawahakikishia kuwa tutapamba kufika Nusu Fainali msimu huu.”

HATARI: Liverpool kumeguka meguka
Mchungaji Mackenzie ni gaidi, afunguliwe mashitaka - Ruto