Wang’amuzi wa vipaji vya soka kwa wachezaji wa Manchester United wameripotiwa kwenda mjini Naples kumtazama Mshambuliaji SSC Napoli, Victor Osimhen ikiwa ni sehemu ya mpango wa kumvuta supastaa huyo wa Nigeria huko Old Trafford mwishoni mwa msimu huu.

Man United imekuwa ikihusishwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya na Osimhen ni moja ya wakali wanaohusishwa na mabingwa hao mara 20 wa Ligi Kuu England.

Osimhen, 24, panga pangua amekuwa kwenye sehemu ya kikosi cha Napoli msimu huu, huku mavitu yake matamu ndani ya uwanja yakiipa timu hiyo nafasi ya kushinda ubingwa wao wa kwanza wa Serie A tangu msimu wa 1989-90.

Timu hiyo inayonolewa na kocha Luciano Spalletti inashika usukani wa Serie A na imeizidi timu inayofuatia kwenye msimamo kwa zaidi ya pointi 10.

Akiwa amefunga mabao 21 katika mechi 24 za ligi, Osimhen amevutia klabu nyingi za Ulaya, huku Man United ikipewa nafasi kubwa ya kunasa saini yake kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Skauti wameanza mchakato wa kumfuatilia kwa karibu mshambuliaji huyo.

Man United jana Jumapili ilikuwa na shughuli pevu ya kuwakabili Brighton uwanjani Wembley katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA.

Gary Neville: Wachezaji watatu Arsenal wajitafakari
Wapiga kelele makazi ya watu kuchukuliwa hatua