Kurejea kwa Wachezaji watatu tegemeo katikakikosi cha Mabingwa wa Soka Barani Afrika Wydad Casablanca, huenda kukaipa wakati mgumu Simba SC katika mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana keshokutwa Ijumaa (Aprili 29) katika mchezo wa Mkonda wa Pili utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mohammed V ambao upo mjini Casablanca nchini Morocco.

Katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopogwa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumamosi (April 22) Simba SC iliibuka na ushindi wa 1-0, bao likifungwana Jean Baleke.

Katika mchezo huo wa marudiano, Wydad Casablanca inatarajiwa kuwatumia wachezaji wake watatu tegemeo waliokosekana kutokana na majeraha ambao ni Mshambuliaji Bouly Junior Sambou, kiungo mshambuliaji Mohammed Ounnajem na Mlinda Lango chaguo la Kwanza Ahmed Reda Tagnaouti ambaye ni Mlinda Lango chao la Pili katika Timu ya Taifa ya Morocco.

Mastaa hao wote juzi Jumatatu (April 24) walionekana katika mazoezi ya timu hiyo, wakijiandaa na mchezo huo wa marudiano dhidi ya Simba SC ambayo tayari imeshawasili mjini Casablanca tangu jana Jumanne (April 25).

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu mjini Casablanca, wachezaji hao wote wapo katika orodha na mipango ya kutumika kuelekea pambano hilo.

Katika hatua nyingine, mtandao wa klabu hiyo umetoa taarifa za kwamba tiketi za mchezo wa huo zimemalizika baada ya kununuliwa zote juzi Jumatatu (April 24) na mashabiki wa timu hiyo.

Hiyo siyo mara ya kwanza kwa mashabiki wa Wydad AC kununua tiketi zote na kuzimaliza kwani walifanya hivyo katika michezo yote ya timu hiyo, ilipokuwa katika hatua ya makundi.

Zoezi la kuwarejesha Watanzania Sudan linaendelea - Dkt. Tax
Wachezaji Simba SC wampa jeuri Robertinho