Klabu ya Chelsea imeanza kuhusishwa na mpango wa kumsajili Mlinda Lango kutoka nchini Cameroon na Klabu ya Inter Milan ya Italia Andre Onana, ili kutibu changamoto ya lango lao.

Kwa sasa lango la Chelsea limekuwa katika utetezi wa Walinda Lango Kepa Arrizabalaga kutoka Hispania na Édouard Mendy kutoka nchini Senegal.

Hata hivyo Chelsea inatajwa kuingia katika vita ya kumuwania Onana, kwa ushawishi wa fungu la Fedha pamoja na kumtoa Mlinda Lango wao Kepa ili ajiunge na Inter Milan mwishoni mwa msimu huu.

Mabosi wa Chelsea wanataka kumsajili Onana mwenye umri wa miaka 27, wakiamini endapo wakimpata Mlinda lango huyo watafanikiwa kwa kiasi kikubwa kutibu tatizo ambalo limekuwa likiwasumbua hasa Kepa anapopewa nafasi ya kulinda Milingoti mitatu.

Onana ambaye msimu huu anaongoza kwa saves (40) na Clean Sheet (6) katoka Ligi ya Mabingwa Ulaya, amekuwa mhilimili muhimu kwenye kikosi cha Inter Milan ambacho amekisaidia kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Mkataba wa sasa wa Mlinda Lango huyo unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, na mabosi wa Inter wanadaiwa kuhitaji kiasi kisichopungua Pauni Milioni 35 ili kumuachia.

Serikali yanunua Ng’ombe 865 vituo nane vya ufugaji
TPBRC yafuta matokeo ya April 22