Kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC, kiungo kutoka nchini Zambia na Klabu ya Simba SC, Clatous Chama amechimba mkwara mzito kwa kusema kikosi chao kitafuzu Nusu Fainali ya michuano hiyo kutokana na faida kubwa ya uzoefu walionao.

Kesho Ijumaa (Aprili 28) Simba SC itakuwa kwenye Uwanja wa Mohamed V jijini Casablanca nchini Morocco kurudiana na wenyeji wao Wydad AC kuwania kufuzu Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakicheza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumamosi (Aprili 22) Simba SC walifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali.

Chama amesema: “Malengo yetu ni kufika nusu fainali, tunawaheshimu Wydad ni miongoni mwa timu bora na ngumu, lakini tumejipanga kupambana kupata matokeo mazuri.

“Faida kubwa kwetu ni uzoefu ambao tunao kwenye mashindano haya na hasa ukizingatia siku chache zilizopita tulikuwa Morocco kwa ajili ya mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya mashindano haya.”

Vijana simamieni maadili, lindeni muungano - Dkt. Mwakyembe
Frankfurt yakanusha kukutana na Bayern Munich