Nahodha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Bakari Mwamnyeto amesema kikosi chao kililazimika kubadili mfumo kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Rivers United, iliyokuwa nyumbani katika Uwanja wa Godswill Akpabio, mjini Uyo nchini Nigeria.

Katika mchezo huo Young Africans ilichomoza na ushindi wa mabao 2-0, yakifungwa na Mshambuliaji kutoka nchini DR Congo Fiston Kalala Mayele.

Kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa Jumapili (Aprili 30) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Mwamnyeto amesema, wapinzani wao hawatakiwi kuhisi chochote kuhusu mpango wao na wasitarajie kama watacheza kama ambavyo walicheza kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza.

“Tuliwaweza wapinzani wetu kwa kubadili mfumo ambao tulianza nao, hivyo tulipata matokeo kwa sababu tulibadilika hadi namna ya ushambuliaji. Kitu ambacho kinakwenda kuwa tofauti kabisa kwenye mchezo wa Jumapili.”

“Mpango wetu kama timu ni kufika fainali, hivyo wapinzani wetu wasitegemee kuona mpira wa namna ile ile tena kwenye mechi ya marudiano, kwetu hii ndiyo mechi ambayo inakwenda kubadilisha historia yetu.’ amesema Beki huyo aliyesajiliwa Young Africans miaka mitatu iliyopita akitokea Coastal Union ya jijini Tanga.

Tanzania, Rwanda kuimarisha usafirishaji, biashara
Inonga amfurahisha kocha Robertinho