Wawakilishi wa Mabingwa wa Soka Barani Ulaya Real Madrid wanatarajiwa kusafiri hadi Ujerumani kwa ajili ya kufanya mazungumzo na mabosi wa Borussia Dortmud juu ya uwezekano wa kuipata huduma ya kiungo wa England, Jude Bellingham katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Jude mwenye umri wa miaka 19, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025 na amekuwa akihusishwa na timu nyingi barani Ulaya ikiwa pamoja na Liverpool.

Ili kumuuza staa huyu wa kiamataifa wa England, Dortmund inahitaji zaidi ya Pauni 100 milioni jambo ambalo limeziengua timu nyingi kwenye dili hilo.

Kwa mujibu wa ripoti mbali mbali ni kwamba Bellingham mwenyewe hataki kujiunga na timu yoyote zaidi ya Madrid katika dirisha lijalo na ikiwa itashindikana ataendelea kusalia Dortmund hadi mkataba wake umalizike mwaka 2025.

Pochettino kumpeleka Harry Kane Chelsea
Wakazi wa Dar chukueni tahadhari ya kipindupindu