Meneja wa Klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp pamoja na timu yake kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham amesema kikosi chake bado kuna shida ya kucheza vizuri katika kila mchezo.

Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham unaifanya timu hiyo kushinda michezo mitatu mfululizo na kutimiza idadi ya michezo mitano bila kufungwa, huku bado wakiwa kwenye nafasi ya kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Liverpool ina nafasi ya kushinda mchezo wake wa nne mfululizo wa Ligi Kuu England kwa mara ya pili msimu huu watakapoikaribisha Tottenham katika dimba la Anfield kesho Jumapili (Aprili 30), lakini kocha huyo kutoka Ujerumani amekuwa makini kutoridhika na kiwango cha hivi karibuni cha timu hiyo.

“Kwa upande wangu ni mapema sana kuzungumzia kwamba timu yangu inacheza vizuri kila mechi,” amesema.

“Kushinda mechi tatu mfululizo kwangu sio kama tumeweza kucheza vizuri kila mechi, inaweza kuwa mwanzo wa kitu fulani.

“Nina furaha kwa wakati huu, lakini sio kama tayari naamini sana kile tunachofankiasi cha kusema kwamba tuko vizuri, kwa sababu ya masomo machache nimejifunza.”

Liverpool inaweza kumaliza msimu kwa kishindo na bado inaweza kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao lakini iko nyuma kwa tofauti ya alama moja na Spurs ambayo inashika nafasi ya tano na nyuma kwa alama saba dhidi ya Manchester United inayoshika nafasi ya nne.

“Kama hatujafanya kitu fulani cha kipekee msimu huu tutakumbukwa kwa ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Manchester United,”

“Nina imani watu watazungumza kuhusu huu ushindi, wakati wataporudi nyuma na kuangalia miaka michache iliyopita. Tulifanya kile tulichofanya.” amesema Klopp

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Aprili 30, 2023
Namungo FC yaisubiri Simba SC Majaliwa Stadium