Wakati Mauricio Pochettino akitajwa kuwa Meneja ajaye wa Chelsea, imebainika kuwa kocha huyo anataka kuunda pacha mpya ya ushambuliaji ndani ya kikosi hicho kwa kuwaunganisha Joao Felix na Romelu Lukaku.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vimeripoti kuwa mipango ya Pochettino ndani ya klabu hiyo ni kuwafanya wawili hao waungane na kutengeneza pacha ambayo itakuwa na manufaa ndani ya kikosi hicho.

Meneja huyo kutoka nchini Argentina anataka kumrudisha kundini Lukaku ambaye alishindwa maisha ndani ya timu hiyo licha ya kusajiliwa kwa gharama kubwa akitokea Inter Milan akiamini anaweza kurudisha makali yake na kuwa msaada mkubwa katika kikosi chake.

Kwa sasa Lukaku yupo Inter aliporudishwa baada ya kuwa na maisha mabaya chini ya kocha Thomas Tuchel wakati akiwa Chelsea na anatazamiwa kurejea klabuni hapo msimu ujao.

Felix yeye alisajiliwa Klabuni hapo kwa mkopo akitokea Atletico Madrid ya Hispania na anaweza kusalia hapo kwa mwaka mwingine zaidi licha ya sasa kuwa na maisha magumu ya kutokucheza kwenye kikosi cha meneja wa muda, Frank Lampard.

Wakazi wa Dar chukueni tahadhari ya kipindupindu
Kocha Singida BS aikomaliza Young Africans