Paulo Dybala ni miongoni mwa mastaa ambao watapatikana huru mwisho wa msimu huu baada ya klabu yake ya AS Roma kuweka wazi kuwa nyota huyo ataondoka klabuni hapo.

Dybala amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha AS Roma msimu huu tangu alipojiunga nayo akitokea Juventus, akiisaidia timu hiyo kutinga Nusu Fainali ya Europa League.

Mshambuliaji huyo kutoka Argentina atapatikana kwa dau Euro Milioni 10.6 kwa timu yoyote ya nje ya Italia na dau la Euro milioni 17.6 kwa timu za ndani ya Italia.

Hadi sasa Dybala ameifungia AS Roma mabao 16 kwenye michezo 34 ya timu hiyo na kuwekwa sokoni kunaweza kuwa habari kwa timu za England ambazo zimekuwa zikihitaji saini yake.

Maafisa watakao husika na ufisadi kufungwa jela
Mgogoro wa Sudani utakuwa jinamizi kwa ulimwengu - Hamdok