Taharuki imeibuka katika Shule ya Sekondari Imenya iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga baada ya Mkuu wa Shule hiyo, Selemani Karavina kudaiwa kupeleka Mganga wa Kienyeji katika shule hiyo kwa ajili ya kupiga ramli.

Kwa mujibu wa Kituo cha habari cha Habari leo, Diwani wa Kata ya Itwangi ilipo Shule hiyo Sonya Mhela amesema Wazazi na Wanafunzi walikuwa katika taharuki na baadhi ya wanafunzi wanadaiwa walianguka hovyo na kupiga kelele.

“Tukio hili limetokea hivi karibuni na mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili aliandikiwa barua na watu wasiojulikana akituhumiwa yeye na wazazi wake ni washirikina hivyo watauwawa” alisema Mhela.

Diwani Mhela alimuomba Mkuu wa Wilaya kuitembelea shule hiyo ili kujionea na kuwatoa wasiwasi wazazi kwani siku moja kiliitishwa kikao cha wazazi na walimu walishindwa kuelewana na kikao kikavunjika.

Kaimu ofisa elimu Sekondari Clensensia Jogopa alisema tukio hilo ndilo analisikia ndani ya kikao cha baraza la madiwani hivyo watalifuatilia na kuchukua hatua.

Mgogoro wa Sudani utakuwa jinamizi kwa ulimwengu - Hamdok
Pochettino kumpeleka Harry Kane Chelsea