Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewaomba Watanzania kuliombea Taifa la Tanzania na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Viongozi wasaidizi wake akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Zuberi Homera na Mbunge Dkt. Tulia Akson kuendelea kuwa na afya, hekima, uvumilivu na baraka katika majukumu ya uongozi.

Malisa ameyasema hayo mara baada kushiriki ibada katika Kanisala la Assembless of GOD Gospel Church International lililopo kata ya Ruanda Mkoani humo na kutumia nafasi hiyo kuwahimiza Wananchi juu ya suala la usafi wa mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Kanisa hilo.

Amesema, serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini kukemea vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kusimamia miradi mikubwa ya maendeleo iliyoletwa na Serikali Mkoani Mbeya ukiwemo wa Ujenzi wa Barabara nne na Mradi wa Maji wa Mto Kiwira.

Sehemu ya Waumini wa Kanisala la Assembless of GOD Gospel Church International.

Kanisa hilo, limefanya maombi maalumu ya kuwaombea Viongozi wa nchi akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake.

Umeme Uwanja wa Mkapa wasimamisha watumishi
NSSF yang'ara maadhimisho usalama, afya mahali pa kazi