Meneja wa Klabu Bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Thomas Tuchel amepanga kufanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi chake kwa msimu ujao na sasa anamtaka Mshambuliaji Ollie Watkins wa Aston Villa kwa ajili ya kuliboresha eneo lake la ushambuliaji.

Tuchel anamtaka Watkins baada ya Muingereza huyo kuwa na kiwango cha juu msimu huu tangu aanze kufundishwa na Meneja Emery aliyetua Aston Villa akichukua nafasi ta Steven Gerrard.

Mshambuliaji huyo huyo chini ya Unai amefanikiwa kufunga mabao 15 ambayo yamemfanya Tuchel kumtazama kama mchezaji wa kumsajili baada ya kuona ugumu wa kumtwaa Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane.

Bayern wameanza kumfuatilia nyota huyo ambapo maskauti wao walikuwepo wakati Aston Villa ilipopambana na Fulham Jumanne juma lililopita.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 2, 2023
Mbadala wa Baleke, Chama kusajiliwa Simba SC