Uongozi wa Singida Big Stars umetuma ujumbe mzito kwa wapinzani wao Young Africans kuelekea michezo miwili mfululizo itakayowakutanisha katika Uwanja wa CCM Liti juma hili.

Singida Big Stars itaanza kuikaribisha Young Africans mjini Singida Alhamis (Mei 04) katika mchezop wa Ligi Kuu Tanzania Baram kisha itaendelea kuwa nyumbani kuwakabili Wananchi katika mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kuchezwa Jumapili (Mei 7).

Afisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza amesema wanatambua uimara wa wapinzani wao lakini hawana hofu kutokana na maandalizi ambayo wanaendelea kuyafanya kuelekea michezo hiyo ambayo amekiri kwao ina umuhimu mkubwa.

“Tunatambua ubora wa wapinzani wetu Young Africans lakini haina maana kwamba tunamashaka hapana ugumu wa ratiba unatufanya tuwe kwenye maandalizi mazuri ya kupata ushindi kwenye mchezo wetu.”

“Wachezaji wapo tayari na wanatambua kuhusu mchezo huo ukizinagatia tulianza kukata tiketi mapema kwenye mashindano haya tukawa tunajua mshindi kati ya Young Africans ama Geita Gold huyo tutakutana naye.”

“Kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kuelekea kwenye mechi zetu za Mei ambazo zitachezwa Uwanja wa Liti ni mara ya kwanza kwetu kucheza nusu fainali ya kombe hili tunahitaji kufika fainali na kutwaa taji,” amesema Masanza

Ruto atangaza kuunda tume kuchunguza Makanisa
Mei Mosi: Serikali yaahidi neema kwa Wafanyakazi