Bondia Karim Mandonga anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Alick Mwenda wa Malawi katika pambano linalotarajia kupigwa Juni 24, mwaka huu kwenye Viwanja vya Chinangale mkoani Dodoma.

Mandonga anapanda ulingoni kwenye pambano hilo ikiwa ni miezi miwili tangu amchape Kenneth Lukyamuzi wa Uganda nchini Kenya katika pambano la kuwania mkanda wa Ubingwa wa PST Afrika Mashariki na Kati.

Mandonga amesema kuwa anatarajia kurejea ulingoni kuzichapa dhidi ya Mwenda wa Malawi katika pambano ambalo litakalopigwa kwa raundi nane.

“Nashukuru Mungu nipo sawa natarajia kurejea ulingoni Juni 24, mwaka huu pale Dodoma, hii kwangu itakuwa ni mara ya kwanza kupigana ndani ya Jiji la Dodoma Mandonga Mtu Kazi, niwaambie mashabiki wangu nakuja huko kufanya maajabu.”

“Huyo Mwenda anatakiwa ajiandae kweli kwa sababu tayari nimeshaingia kambini kwa ajili ya pambano hilo, anatakiwa kujua nishapiga watu nje na kuipa sifa kubwa Tanzania basi na yeye nitampiga na kuendelea kuipa sifa nchini yangu katika pambano langu hilo,” amesema Mandonga

Madaktari waanza upasuaji miili 109 mfungo wa kifo
David Milandu kutikisa usajili Tanzania Bara