Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Zanzibar, Tabia Maulid Mwita amewataka wanahabari kufuatia habari kwa uhakika ili wananchi waweze kupata taarifa sahihi na kwa wakati ikiwemo kuzingatia suala la uwajibikaji wa kazi zao kwa weledi

Waziri Tabia ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la siku mbili la kuadhimisha miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, na kuongeza kuwa habari ni kitu muhimu hivyo wanahabari wana jukumu la kutoa taarifa sahihi kwa jamii na kujitahidi kufanya kazi zao  kwa weledi.

Amesema, “siku ya uhuru wa vyombo vya habari inatoa fursa kwa watu duniani  kote hasa wanahabari kuonyesha mshikamano wao kwa kutoa wito wa kuondoa vizuizi vya kupata habari.

Aidha, Waziri huyo pia ameongeza kuwa Wanahabari wanao uwezo wa kudai uwajibikaji kutoka kwa viongozi na Taasisi kwa kuwakumbusha watu kuhusu umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika kukuza maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Mrajisi Vyama vya Ushirika akali kuti kavu
Tanzania yatwaa Medali michuano ya Afrika