Baada ya kutinga Nusu Fainali ya Kombe Shirikisho Barani Afrika Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi, amesema kuwa sasa ameanza kuwapigia hesabu wapinzani wao Mallumo Gallants.

Mallumo wametinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kuiondoa Pyramids kwa mabao 2-1 wakianza na sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa 30 June Misri na baadae kushinda 1-0 nchini Afrika Kusini.

Young Africans juzi Jumapili (Aprili 30) ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ikiwa ni timu ya kwanza kutoka nchini Tanzania, kutinga hatua hiyo baada ya kuibuka na jumla ya ushindi wa mabao 2-0 na Rivers United.

Nabi amesema mechi yao ilikuwa ya ushindani mkubwa kwa sababu alitambua wapinzani wake hao wangekuja kucheza na ikamlazimu kucheza kwa kukaba zaidi.

“Mechi ilikuwa ngumu tangu awali nilisema kuwa Rivers hawana cha kupoteza wangecheza mpira, ikatulazimu kucheza kwa kuzuia kwa sababu ningefunguka wangepata bao la kwanza na baadae wangefunga la pili.

“Nimeshafahamu nitakutana na Marumo Gallants, hivyo itanilazimu kabla ya kuanza mipango ya mechi hiyo lazima niwafuatilie wapinzani wangu ubora na madhaifu yao,” amesema Nabi.

TZ Prisons yaichongea Mbeya City Ligi Kuu
TFF yasogeza mbele Nusu Fainali ASFC