Aliyekuwa Mshambuliaji mahiri wa Liverpool Michael Owen ameutaka Uongozi wa Klabu hiyo kumsajili kiungo wa West Ham United, Declan Rice kama itashindwa kumnasa kiungo nyota wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham anayewaniwa na Real Madrid.

Rice anayekipiga West Ham na timu ya taifa ya England, amekuwa akihusishwa kuwaniwa na klabu mbalimbali zikiwemo Arsenal, Chelsea na Manchester United.

Mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao 2023/24.

Liverpool kwa muda mrefu imekuwa ikimuwania Bellingham ambaye hivi karibuni ameripotiwa kukaribia kutua katika klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

Owen amesema kama Liverpool itashindwa kumnasa Bellingham, inapaswa imnase Rice au mchezaji mwingine mwenye ubora wa juu.

Owen ambaye aliwahi kukipiga Liverpool, alisema ikiwa klabu hiyo itashindwa kumnasa Bellingham, basi inapaswa kumsajili Rice au anayefanana naye ili kuimarisha kikosi chao msimu ujao.

“Nenda ukamsajili (mchezaji) bora nayefuata, jaribu kumnasa Declan Rice au mpate mwingine ambaye ana uwezo wa juu,” amesema Owen mwenye umri wa miaka 43.

Kiungo huyo amefunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za mabao katika michezo 33 aliyocheza katika Ligi Kuu ya England msimu huu 2022/23.

Rais aipa pole familia ya Waziri aliyeuawa kwa risasi na mlinzi wake
Samir aipa Tanzania Medali ya pili Afrika