Klabu Bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain kuelekea msimu ujao, imeweka mipango kwa kufanyia kazi maeneo manne muhimu, ili kufanikisha malengo iliyojiwekea.

Paris Saint-Germain imejipanga kurekebisha kikosi hicho na kuhakikisha msimu ujao kinakuwa imara na bora zaidi, kwa ajili ya Michuano ya ndani na nje ya Ufaransa.

Katika kuhakikisha hilo, wamejipanga kusajili Mshambuliaji mmoja wa daraja la juu ambaye atakuwa na msaidizi wake.

Lakini pia wanataka kusajili Kiungo Mshambuliaji upande wa kushoto ambaye ana ubora, atakayeisaidia klabu hiyo katika mapambano yake.

Huku eneo la kiungo mkabaji ataletwa fundi pia ili kuhakikisha timu inacheza kwa kiwango bora na cha juu. Paris Saint-Germain kwa maana hiyo ina mpango wa kusajili wachezaji wanne msimu ujao.

Lakini taarifa zinaeleza kuwa kuna wachezaji ambao watauzwa ndani ya kikosi hicho na wengine huenda wakatolewa kwa mkopo.

Watendaji Halmashauri watakiwa kukamilisha miradi kwa wakati
Maji yamezidi unga jijini Paris Ufaransa