Tajiri wa Qatar Hamad bin Jassim bin Jaber bin Mohammed bin Thani Al Thani amedhamiria kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na Klabu ya PSG Kylian Mbappe, endapo atapata ridhaa ya kuimiliki Klabu ya Manchester United kwa kitita cha Pauni Bilioni 5.

Wachezaji wengine wanaotajwa huenda wakatua Old Trafford chini ya utawala wa Kibopa huyo ni wale wa wanaozitumikia klabu za Bayern Munich na Real Madrid.

Sheikh Jassim ambaye pia ni Mwanasiasa nchini Qatar anaongoza katika kinyang’anyiro cha kuchukua mikoba ya kuimiliki Manchester United na tayari nyota kama Kingsley Coman na Eduardo Camavinga pia wanaripotiwa kulengwa kwenye mipango ya kuwanunua.

Hadi sasa Jassim anashindana na Sir Jim Ratcliffe katika harakati za kuinunua United kutoka familia ya Glazers.

Sheikh Jassim anataka kumnunua Kylian Mbappe kutoka Paris Saint-Germain mara tu atakapokamilisha mchakato wa kuinunua Manchester United.

Tajiri wa Qatar Hamad bin Jassim bin Jaber bin Mohammed bin Thani Al Thani

Kibopa huyo ni mmoja wa vyama viwili vinavyofikiriwa kuwa miongoni mwa wagombea wakubwa pamoja na Sir Jim Ratcliffe wanaposhindana kununua hisa kubwa ya Old Trafford kutoka kwa familia ya Glazer.

Hata hivyo Mbappe amesaini mkataba na PSG hadi msimu wa joto wa 2024.

Kocha Tanzania Prisons azitaka alama tisa Ligi Kuu
Kesi vifo vya waumini: Mchungaji Odero aachiliwa kwa dhamana